Sunday, April 21, 2013

huyu ndo Mwalimu Nyerere alisema tumuogope kama ukoma

Nimeshangaa sana chama kinakuwa na watu wenye confidence ya kufanya mambo yasiyo sawa kupitia kutoa kauli mbovu,alafu wanashangiliwa sana na wasiojua matokeo ya kauli hizo, hapa hakuna usalama hata kidogo, hii haina usalama ndani yake , hizi kauli za kijinga hasa kutoka kwa wale wanaofikiria kuwa kaskazin ndo bora kuliko sehem nyingine za tanzania nasema wamepotoka saana, huo msimamo wa majimbo na kutaka kujitenga si msimamo mzuri kwa nchi ambayo bado tunamatatizo ya njaa, rushwa, uwajibikaji mdogo, sasa mnataka kutuongezea mzigo wa kutatua tatizo la ukabira na ujimbo, yaan mnaweza kujitenga hasa kwa ulevi wa madaraka na sera za vijiwen lakin jua hamtabaki salama, maana mnaojiita wa kaskazini na mkawabagua wa kusini mtajikuta kumbe si wamoja maana kuna wachaga, wapare, wa barbaig, wa arumeru, wa masaai, wa irak,eee,ni weng sana sasa mtakuta kuna WAKASKAZINI NA WAKASIKUSIN maan bila kupata msaada wa kusini kuna ambao hawata survive, MI NAONA HUYU TUMUOGOPE KAMA UKOMA KAMA ALIVYOSEMA MWALIMU NYERERE

Wanasiasa kikwazo shughuli za vikoba/ WANAKWAMISHA WANAOTAKA KUJIAJIRI

WANASIASA nchini wamedaiwa kuingilia shughuli za benki za vijijini (vikoba), hivyo kuwafanya wananchi kushindwa kujikwamua katika hali ngumu ya umaskini.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa waratibu wa mkoa wa vikoba, Edward Mlowe, katika mkutano wa taifa wa robo mwaka uliofanyika ukumbi wa Princes, Sinza, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali.
Mlowe alisema kikwazo hicho kwa wanasiasa kinakuja pale wanapoitisha mikutano ya kutaka kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na vikundi hivyo lakini cha kushangaza wanawahadaa kutoshiriki kwa kuhofia kwamba huenda kuna mpinzani mwenzao katumia vikoba kuwarubuni wananchi wake.
Hata hivyo mratibu huyo alisema maeneo ambayo yamekuwa yakitokea matukio kama hayo ni kwa wakuu wa mikoa ambao wamekuwa wakiwapa ushirikiano wa kutosha.
Mwenyekitii wa Vikoba taifa, Teddy Sanga, alitaja changamoto nyingine wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu na mitaji kwa wanachama.
Ili kukabiliana na hali hiyo alisema vikoba imekuwa ikitoa elimu ya ujasiriamali kwa wanachama hao ili kusaidia kuwabadilisha kifikra na kimtazamo na kujitambua kwamba kwa kiasi kidogo cha fedha walichonacho wanaweza kuanzisha hata biashara ndogondogo ambazo baadaye zinakuja kuwa kubwa.
Diwani wa Kata ya Yakobi, mkoani Mbeya (CCM), Ester Mgeni, alisema Vikoba katika Mkoa wao imewasaidia wananchi wengi kuondokana na umaskini.
“Wanasiasa wenzangu wanapaswa kuelewa kwamba huwezi kumuongoza mtu ambaye ni maskini, hivyo vikoba ni moja ya eneo maalumu ambalo litawawezesha wananchi wetu kuondoka huko walipo na kuwa watu ambao wataweza kujiendeleza kimaisha,” alisema Mgeni.